2326; Dalili za kuangalia kwa watu sumu…
Umesikia sana kuhusu watu sumu, watu wa kuwaondoa kwenye maisha yako kwa sababu ni kikwazo kwako.
Kuna dalili muhimu za kuangalia kwa kila mtu na ukiziona basi jua ni sumu na unapaswa kuwa nao mbali.
- Je unajisikia vibaya au kuwa na wasiwasi baada ya kutumia muda wako na watu hao?
-
Je unapokuwa nao mnaishia kubishana kwenye kila jambo kuliko kuishia kuelewana?
-
Je wanajaribu kukushusha chini au kukukandamiza ili usioige hatua zaidi?
-
Je wanakuzibia baadhi ya fursa ili usizipate au kunufaika nazo?
-
Je wanatengeneza fitina kati yako na watu wengine ili kuharibu mahusiano yako na watu hao?
-
Je wanayaonea wivu mafanikio yako au kujaribu kushindana na wewe ili kuangusha mafanikio yako?
-
Je hawakusikilizi kama wewe unavyowasikiliza?
-
Je ni watu wa kuleta kila aina ya mikasa kwenye maisha yako?
-
Je wanataka uwajali zaidi wao kiasi hata cha kupuuza mambo muhimu kwako kama afya yako?
-
Je huwa unajikuta unaishia kulia kila unapowapa watu hao muda?
Kama jibu ni ndiyo kwenye swali lolote hapo, basi jua umekutana na mtu sumu na jihadhari naye sana.
Watu hao ndivyo walivyo, huwa hawabadiliki, hivyo kilicho sahihi kwako ni kuachana nao mara moja, usijiulize zaidi.
Kocha.