
Huwa tunawalalamikia watu kwamba wamebadilika, wakati tunaanza nao mahusiano au ushirikiano walikuwa namna fulani ila baadaye tunaona wamebadilika na kuwa kikwazo.
Ukweli ni kwamba watu siyo wamebadilika, bali wameonesha uhalisia wao, wamekuwa hawawezi tena kuendelea kuficha uhalisia wao.
Lakini tangu awali, kuna viashiria ambavyo watu walikuwa wanatuonesha ambapo kama tungevizingatia, tungeweza kuwajua ni watu wa aina gani.
Watu wanaweza kuficha makucha yao, lakini kuna viashiria huwa havifichiki, vinakuwa wazi kabisa. Na sauti yako ya ndani inakueleza wazi, ila wewe kwa kutaka sana kuwa au kushirikiana na mtu huyo, unapuuza. Ni mpaka baadaye, wakati hisia ulizokuwa nazo awali zimeisha ndiyo unaona ukweli kama ulivyo.
Usipuuze viashiria vyovyote unavyoviona kwa watu, usiipuuze sauti ya ndani yako inapokupa tahadhari juu ya watu.
Hapa kuna dalili muhimu za kuangalia kwa watu sumu unaopaswa kuachana nao; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/14/2326
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma