Moja ya nadharia ya mageuzi (evolution) ni kwamba kiungo cha mwili kinachotumiwa sana kinakuwa imara na kile kisichotumiwa kinakuwa dhoofu.

Ndiyo maana kama unatumia sana mkono wa kulia, unakuwa na nguvu kuliko wa kushoto.

Kadhalika ndivyo ilivyo kwenye akili, ukiitumia sana inakuwa imara, usipoitumia inakuwa dhoofu.

Akili dhoofu haiwezi kufanya maamuzi sahihi na haina ubunifu. Wengi hatutumii akili zetu kwa sababu tunaendesha maisha yetu kwa mazoea.

Matokeo yake ni akili zinadhoofu na kushindwa kufanya chochote nje ya mazoea.

Mwandishi James Altucher huna anaita akili ni mashine ya kuzalisha mawazo na kila siku anaandika mawazo kumi juu ya kitu chochote kile. Nilijifunza kwake hili miaka 5 iliyopita ila nilifanyia kazi mara chache tu.

Sasa nimejifunza tena kwake na nimeamua nilifanyie kazi kila siku. Kila siku nitaandika mawazo kumi ya kuingiza fedha kwenye eneo lolote lile na kuweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/21/mawazo