2336; Mtazamo Na Matendo…

Wengi husubiri mpaka wawe na mtazamo au hisia sahihi ndiyo wachukue hatua.
Husubiri mpaka wawe na hamasa ndiyo waanze kufanya.

Lakini hivyo sivyo mambo yanavyofanya kazi.
Mtazamo na hisia havitangulii matendo, bali matendo ndiyo yanatangulia mtazamo.

Kwa kuchukua hatua, unashawishi mtazamo na hisia zinazoendana na hatua hizo.
Kwa kufanya unajenga hamasa ya kuendelea kufanya.

Hivyo usisubiri mpaka upate hamasa ndiyo ufanye unachotaka, bali anza kufanya na utajenga hamasa ya kukusukuma kuendelea zaidi.

Kila mtu anaweza kujenga mtazamo, hisia na hamasa yoyote anayotaka kama tu atachukua hatua zilizo sahihi.

Usisubiri hamasa ndiyo ufanye, anza kufanya na utajenga hamasa.

Kocha.