
Unapoenda kununua kifaa chochote kipya, huwa unapewa kitabu chenye maelezo ya uwezo wa kifaa hicho na jinsi ya kukitumia. Unaposoma kitabu hicho, unaweza kutumia kufaa hicho kwa uwezo wake.
Kwa bahati mbaya binadamu huwa hatuzaliwi na vitabu vya maelezo ya uwezo wetu mkubwa na tunayoweza kufanya. Hicho ni kitu mtu anaweza kukitambua mwenyewe baada ya kujitafuta sana ndani yake.
Wengi wanaishi maisha yao yote bila kujitambua na kuweza kutumia uwezo wao mkubwa.
Wewe usikubali kuwa na maisha ya aina hiyo, jitafakari, sikiliza nafsi yako na jaribu mambo mbalimbali na makubwa ili uweze kujua yale unayopenda na uwezo ulio ndani yako.
Ukurasa wa kusoma ni shamba lisilolimwa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/23/2335
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma