2343; Siku moja haipo…

Kama kuna mpango wowote unaojiwekea kwa siku zijazo na kujiambia siku moja utakuwa umefikia hatua fulani jua unajidanganya.

Hakuna siku yoyote ya mbele inayoitwa siku moja, ndiyo maana huwezi kuifikia.

Badala ya kuacha mipango yako wazi na kutegemea siku moja inayo utakuwa umeifikia, chagua siku ya uhakika, siku yoyote na amua hiyo uwe umekamilisha lengo fulani.

Chagua kabisa ni tarehe ipi utakuwa umekamilisha, kisha anza kuchukua hatua ili tarehe hiyo inapofika uwe umelifikia lengo lako.

Unapoichagua tarehe kabisa unakuwa umefanya maamuzi ya uhakika na kinachofuata ni utekelezaji.
Unapokuwa huna tarehe ya uhakika utaendelea kujiambia siku moja, siku ambayo haipo.

Kocha.