Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ukalimani wa lugha.

Kadiri dunia inavyoungana na kushirikiana, watu wanahitaji kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali.
Lakini lugha huwa ni kikwazo katika ushirikiano huo.

Hapo inajitokeza fursa ya ukalimani, ambapo mtu anayezielewa vizuri lugha mbili, anaweza kusaidia kwenye mawasiliano.

Hapa ni njia kumi za kuingiza kipato kupitia ukalimani wa lugha mbalimbali.

  1. Kuajiriwa na taasisi au makampuni kwa ajili ya kutoa huduma za ukalimani.

  2. Kujiajiri mwenyewe kwenye kutoa huduma za ukalimani kwa mtu mmoja mmoja au taasisi.

  3. Kuwafundisha wengine moja kwa moja lugha ambayo unafanyia ukalimani.

  4. Kuandika kitabu cha lugha unazofanyia ukalimani.

  5. Kuwa na blogu inayohusu lugha na tamaduni mbalimbali za lugha unazofanyia ukalimani.

  6. Kutafsiri kitabu kutoka lugha moja kwenda nyingine.

  7. Kuwasaidia wafanyabiashara katika majadiliano mbalimbali yanayohusisha lugha ambazo hawajui.

  8. Kuwa na taasisi inayofundisha lugha na tamaduni baina ya jamii unazofanyia ukalimani.

  9. Kurekodi sauti na video za kufundisha lugha na kuziuza kwa wengine.

  10. Kuwa mwongozaji wa watalii kwenye maeneo mbalimbali na kuwasiadia mawasiliano.

Kuna fursa kubwa kwenye eneo la ukalimani ambayo mtu anaweza kufanyia kazi na kuingiza kipato kikubwa.
Muhimu ni mtu uwe mbobezi kwenye lugha husika na kutoa thamani kubwa huku ukiwa mwaminifu mkubwa.

Kocha.