Ni rahisi kuona maisha ya wengine ni mazuri kuliko yako.

Ni rahisi kuona kazi au biashara za wengine zinalipa kuliko unayofanya wewe.

Ni rahisi kuona mahusiano ya wengine ni yenye furaha kuliko ya kwako.

Lakini usichojua ni kwamba, kwa wengine unaona upande mmoja tu wa mazuri, wakati kwako unaona upande wa mazuri na mabaya.

Watu ni waigizaji wazuri, wanapenda kuonesha mambo ni mazuri kwa nje, wakati kwa ndani mambo huwa ni tofauti kabisa.

Na mitandao ya kijamii ndiyo imeharibu kabisa, utaona wengine wakipost maisha yao mazuri na kudhani hayo ndiyo maisha yao halisi na ya kila siku, kumbe ni sehemu ndogo mno ya maisha yao.

Maisha halisi ni magumu, yenye changamoto nyingi na yanayochosha. Maisha ya kuigiza yamejaa mbwembwe kibao.

Ukurasa wa kusoma ni uhalisia hauna mbwembwe; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/07/2350

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma