Watu wengi huendesha maisha yao kama vile bado wapo kwenye majaribio au mazoezi ya kuja kuishi maisha yenyewe.

Kila wakati wanaahirisha kuishi, wakiwa shule wanajiambia wataanza kuishi wakihitimu na kupata kazi. Wakipata kazi wanajiambia wataanza kuishi wakistaafu. Wakistaafu wanajikuta wameshachelewa na wanakufa.

Maisha yako ndiyo hayo unayoyaishi sasa, hakuna siku nyingine ambayo ndiyo utaanza kuishi. Kila siku inayopita ni maisha ambayo yameondoka na hayarudi tena.

Hivyo ishi maisha yako kwa ukamilifu wake, kuwa halisi kwako na fanya yale tu yenye tija kwa maisha yako.

Ukurasa wa kusoma ni kuweza kutabiri mafanikio ya biashara; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/10/2353

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma