
Huwa tunafikiri tutayafurahia maisha baada ya kupata vitu fulani au kufika hatua fulani. Tunaharakisha kufika huko na hatuipati hiyo furaha.
Furaha haipo kwenye matokeo, bali kwenye mchakato. Hivyo unapaswa kuweka umakini wako kwenye kile unachofanya, kiwe ndiyo muhimu kabisa na kukipa muda wa kutosha.
Kila unapochagua kufanya kitu, kinapaswa kuwa ndiyo kilicho muhimu kuliko vingine vyote. Na kama ndiyo kilicho muhimu kabisa, basi unakifanya kwa umakini mkubwa na usikiharakishe pasipo na sababu za msingi.
Ukurasa wa kusoma ni unakimbilia wapi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/17/2360
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma