Wakati wengine wanazichukoa na kuzikimbia changamoto, wewe unapaswa kuzifurahia na kuzikaribisha, kwa sababu ndani yake huwa zina fursa nzuri za ukuaji zaidi kwako.

Hutaweza kuziona fursa hizo nzuri kama utaona changamoto ni mbaya. Hivyo anza na mtazamo kwamba changamoto ni nzuri kisha jiulize ni fursa zipi nzuri zilizo ndani ya changamoto hiyo. Utaziona fursa nyingi nzuri unazoweza kutumia na ukapiga hatua zaidi.

Bila changamoto huwezi kupiga hatua kwenye maisha yako, utaishi kwa mazoea ba kubaki ulipo. Changamoto zinakuondoa kwenye mazoea na kukusukuma ufanye mambo ya tofauti.

Zipende changamoto na tafuta fursa zilizo ndani yake.

Ukurasa wa kusoma ni fursa zilizo ndani ya changamoto; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/19/2362

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma