2365; Ingekuwa rahisi, kila mtu angefanya…

Kama inanibidi nifanye maamuzi ya haraka kwenye kitu ambacho sina taarifa za kutosha, huwa ninaangalia aina ya watu wanaokubaliana na kitu hicho au kukipigia debe.

Nikiona watu wengi wanakubaliana nacho na kukisifia, naweza kuwa na uhakika kwamba kitu hicho siyo bora na kinachoweza kumfikisha mtu kwenye makubwa.

Mafanikio siyo rahisi na ndiyo maana wengi hawayapati, maana wengi hupenda vitu rahisi.

Mafanikio yanahitaji kujitoa, kuumia na kuwa na subira, kitu ambacho wengi hawakiwezi.

Mafanikio yanataka mtu kushika hatamu ya maisha yake na kuacha kulalamika na kulaumu, kitu ambacho wengi hawakiwezi.

Waambie walioshindwa kwamba uzembe wao ndiyo umewafikisha walipo na watakuchukia kabisa. Waambie ni serikali imefanya wawe walipo na watakupenda.

Wachache wanaoweza kuupokea ukweli unaoumiza na kuufanyia kazi, ndiyo wanaoweza kupata mafanikio makubwa.

Je wewe uko upande wa wachache walio tayari kwa magumu ili kuweza kufanikiwa?

Kocha.