Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ufugaji wa kuku.

Kuku ni moja ya vitoweo ambavyo vimekuwa vinatumiwa na binadamu kwa muda mrefu.
Wapo wanyama wengi wanaoliwa, ila ni nyama ya kuku ndiyo isiyokuwa na udhibiti kwa wengi.
Watu wanaweza kunyimwa wasile nyama ya ng’ombe kwa sababu za kiafya, ila siyo ya kuku.

Kwa uhitaji na matumizi yake, ufugaji wa kuku unatoa fursa kwa wengi kuweza kuingiza kipato kizuri.
Hapa ni mawazo kumi ya kuingiza fedha kwa kutumia ufugaji wa kuku.

  1. Kufuga kuku wa nyama na kuuza.

  2. Kufuga kuku wa mayai na kuuza.

  3. Kuwa na mashine ya kutotolesha vifaranga na kuviuza kwa wengine.

  4. Kuwatoza watu kuwatotoleshea vifaranga kwa mashine.

  5. Kuuza vyakula vya kuku.

  6. Kuuza madawa na chanjo za kuku.

  7. Kuuza mbolea inayopatikana kwenye ufugaji wa kuku.

  8. Kusindika na kuuza nyama ya kuku.

  9. Kununua kuku wa kienyeji vijijini na kuuza mjini.

  10. Kuendesha mafunzo na ushauri wa ufugaji wa kuku.

Kocha.