
Huhitaji kufanya ugunduzi mkubwa au mapinduzi fulani ndiyo uache alama hapa duniani.
Ipo njia rahisi ambayo kila mmoja wetu anaweza kuitumia na akaacha alama kubwa. Njia hiyo ni kujifunza kwa kupata maarifa sahihi, kuyatumia maarifa hayo ili kuyafanya maisha yako kuwa bora kisha kuwafundisha wengine kile unachojia na uzoefu uliopata.
Chukua mfano upo kwenye madeni yanayokutesa, ukajifunza jinsi ya kuondokana nayo, ukachukua hatua na kuondoka kwenye madeni hayo, halafu ukawafundisha wengine nao wakaondoka kwenye madeni, utakuwa umegusa sana maisha yao na kuacha alama kubwa, hawatakusahau.
Usijiambie huna namna ya kuibadili dunia, anza kujibadili wewe na shirikisha uzoefu wako kwa wengine.
Ukurasa wa kusoma ni jifunze, nufaika, fundisha; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/21/2364
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma