2367; Ngwe nyingine….

Igawe siku yako kwenye ngwe mbalimbali.
Hiyo itakusaidia pale unaposhindwa kufanya ulichopanga, badala ya kusema utakifanya kesho, jiambie utakifanya kwenye ngwe nyingine.

Huwa unaanza siku kwa kuipanglia vizuri, lakini huwa yanatokea mambo na kuvuruga mipango yako.
Ni rahisi kuona siku imeharibika na kujiambia utafanya tena kesho.
Lakini kesho ni mbali na inaweza isifike.

Hivyo kila ratiba yako inapovurugwa, usiisukume kwenda kesho, bali isogeze kwenda mbele.
Maliza usumbufu uliokuingilia na kisha rudi kwenye ratiba yako.

Ngwe unazoweza kuzigawa kwenye soku yako ni alfajiri, asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku.
Kama kuna ratiba ulipanga ufanye asubuhi ila ikavurugika, usijiambie utafanya kesho, kama ni muhimu fanya kwenye ngwe inayofuata.

Fuata hili na kila siku yako itakuwa bora, ukikamilisha yote muhimu na kupata matokeo mazuri.
Ni kuangalia kwa ngwe zilizo kwenye siku na siyo kuangalia kwa siku nzima.

Usiruhusu usumbufu wowote uvunje ratiba zako, badala yake pambana ukamilishe ratiba zote ulizopanga.

Kocha.