
Ukweli mara nyingi huwa unaumiza na wengi wanaokujali hawapo tayari kukuumiza, hivyo wanaweza kuuona ukweli ila wasikuambie.
Watu wakishagundua hupendi ukweli unaokuumiza, wanakulisha uongo, ili tu ujisikie vizuri. Lakini uongo huo haukusaidii zaidi ya kukupoteza.
Unachohitaji sana ni kuujua ukweli, hata kama unakuumiza, maana huo ndiyo unaokuweka huru.
Tafuta watu waliotayari kukuambia ukweli hata kama unakuumiza, hao ndiyo watakusaidia kuona kile ambacho peke yako huwezi kuona.
Ukurasa wa kusoma ni mtu sahihi wa kusikiliza ukosoaji wake; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/23/2366
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma