Unapopanga kufanya kitu, chukuli kwamba hakuna kesho na pambana ukifanye kama ulivyopanga.

Ni rahisi kujishawishi na kukisogeza mbele kile ulichopanga kufanya, lakini ukisharuhusu hilo, itakuwa vigumu kwako kufanya kitu hicho.

Panga na fanya kama ulivyopanga na kama kutakuwa na usumbufu unaokuzuia usifanye, panga kufanya siku hiyo baada ya usumbufu kuisha na siyo kujiambia utafanya kesho.

Kesho unaweza kuiona ni karibu, lakini huwa haifiki. Leo ndiyo leo, ukipanga fanya na siyo kuahirisha.

Ukurasa wa kusoma ni ngwe nyingine; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/24/2367

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma