Uhuru bila ya nidhamu ni sawa na gari bila ya breki, linaweza kukupeleka kasi sana, lakini kasi hiyo itakupoteza kabisa, kwa sababu huna namna ya kulidhibiti gari.

Watu wengi wamekuwa wanakimbilia kuwa huru kabla hawajajijengea nidhamu na kinachotokea ni wanapotezwa kabisa na uhuru wanaokuwa wamepata.

Wewe pambana kujijengea kwanza nidhamu kabla hujatafuta uhuru zaidi. Uhuru ni kama moto, usipoweza kuudhibiti unageuka kuwa majanga.

Ukurasa wa kusoma ni uhuru siyo rahisi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/25/2368

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma