2373; Usichezee ‘Matirio’…
Kila kitu unachokutana nacho kwenye maisha yako, ni ‘matirio’ ambayo unaweza kutumia kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usikubali kupoteza chochote unachokutana nacho, badala yake kitumie kwa namna yenye manufaa kwako.
Huwa unakula chakula, kinaenda tumboni na kumeng’enywa, virutubisho muhimu vinafyonzwa mwilini na uchafu kuondolewa.
Hivyo ndivyo unapaswa kufanya kila eneo la maisha yako liwe, liweze kuchakata kila unachokutana nacho, uchukue yenye manufaa na kuachana na yasiyo na manufaa.
Usipoteze chochote kinachokuja kwako, kiwe kizuri au kibaya, unachopenda au usichopenda.
Wewe angalia ni kwa namna gani unaweza kutumia kwa manufaa na tumia kwa namna hiyo.
Watu wawili walio kwenye eneo moja na wanaokumbana na kitu kimoja, mmoja anaweza kukitumia vizuri na akanufaika na mwingine akashindwa kukitumia vizuri na kubaki kulalamika.
Usiwe wa kulalamika, kuwa wa kutumia kila kinachokuja kwako kwa manufaa.
Kocha.