
Kwa kawaida huwa hatupendi kufanya vitu vigumu, badala yake tunakimbilia kwenye vitu rahisi.
Sasa kwa kuwa vitu rahisi kila mtu anafanya, vinakosa thamani na inakuwa vigumu kufanikiwa.
Moja ya kazi ngumu ambayo huwa tunaitoroka ni kufikiri na akili zetu huwa zinatafuta kila aina ya sababu ili tu tusifikiri mambo magumu.
Lazima uweze kudhibiti akili yako ili uweze kufikiri mambo magumu na yatakayokupa manufaa makubwa.
Ukiweza kufikiri mambo muhimu na magumu, utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Ukurasa wa kusoma leo ni mapendekezo, siyo amri; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/02/2375
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma