Wengi wanapoyaangalia mafanikio, wanachoangalia ni wanakwenda kupata nini.

Huo ni upande mbaya wa kuangalia maana ndiyo ambao kila mtu anauangalia na ndiyo maana wengi hawafanikiwi.

Wewe angalia kwanza upande wa unatoa nini. Uko tayari kutoa nini ili uweze kufanikiwa?

Mafanikio siyo rahisi na ndiyo maana wengi hawafanikiwi. Kikwazo kikubwa ni mtazamo wa kupata kuliko kutoa.

Ukiwa na mtazamo sahihi wa kuwa tayari kutoa kabla hujaangalia unachopata, utaweza kupata mafanikio makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni mwenza wa uhuru; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/04/2377

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma