Mafanikio makubwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwenye maisha yako, hupaswi kuruhusu kitu kingine kuingilia kipaumbele hicho.

Utaona wengine wakihangaika na mambo mbalimbali kwenye maisha na kutamani kufanya kama wao.

Lakini jua wengi hawafiki kwenye mafanikio makubwa na sababu kuu ni kuhangaika na mambo mengi badala ya kuweka vipaumbele sahihi.

Kwenye maisha unapata kile unachokipa kipaumbele na unapotawanya nguvu zako, huwezi kupata matokeo unayoyataka.

Weka vipaumbele sahihi kisha komaa na vipaumbele hivyo huku ukipuuza mengine yote ambayo hayaendani na kile unachotaka.

Wengine watakuona kama vile hujali, lakini wewe kufikia mafanikio makubwa kutakupa nafasi ya kujali zaidi.

Muda na nguvu zako ni rasilimali zenye ukomo, usizitawanye sana, zikusanye kwenye vipaumbele sahihi ili kuzalisha matokeo makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni kuacha anasa zisizo saizi yako; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/09/2382

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma