Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa matunda.

Matunda ni hitaji muhimu kwa afya ya mwanadamu. Yana vitamini muhimu kwa afya bora na kinga ya mwili.

Kwa uhitaji huu mkubwa wa matunda, kunatoa fursa ya watu kuweza kuingiza kipato kupitia biashara hiyo.

Hapa ni mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia matunda.

  1. Kufanya kilimo cha matunda na kuyauza jumla na/au rejareja.

  2. Kununua matunda shambani na kwenda kuuza jumla na/au rejareja.

  3. Kununua matunda sokoni na kuuza kwa rejareja.

  4. Kuandaa matunda na kuweka kwenye vyombo kwa ajili ya mtu kutumia moja kwa moja.

  5. Kutengeneza juisi ya matunda na kuuza.

  6. Kuyachakata matunda na kuyasafirisha maeneo mbalimbali.

  7. Kuyahifadhi matunda kwa namna ambayo yatakaa kwa muda mrefu na kuyauza bei nzuri kipindi ambacho siyo cha msimu.

  8. Kufundisha na kushauri wengine kwenye kilimo cha matunda.

  9. Kuandika vitabu na kutoa mafunzo kuhusu utumiaji wa matunda na kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji mpaka utumiaji wa matunda.

  10. Kuwa na kiwanda cha kuchakata matunda na kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Fursa ni nyingi kwenye matunda na kadiri watu wanavyokuwa na uelewa na kujali afya zao, ndivyo fursa zinavyozidi kuongezeka.

Kocha.