Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia samaki.
Samaki ni moja ya kitoweo muhimu kwenye maisha ya kila siku.
Kwa kuwa kadiri watu watakavyoendelea kuwepo wataendelea kula, samaki ni moja ya chakula wanachohitaji.
Hapa kuna mawazo kumi ya kuweza kuingiza kipato kupitia samaki.
- Kufuga samaki na kuwauza kwa ajili ya kula.
-
Kufuga samaki na kuzalisha vifaranga kwa ajili ya kuuza.
-
Kuvua samaki na kuuza kwa jumla na/au reja reja.
-
Kutoa mafunzo ya ufugaji wa samaki.
-
Kuwa na kiwanda cha kuchakata nyama ya samaki.
-
Kutengeneza na/au kuuza chakula cha samaki.
-
Kujenga mabwawa na miundombinu mizuri ya ufugaji wa samaki.
-
Kuandika vitabu kuhusu ufugaji wa samaki.
-
Kununua samaki kwa jumla kutoka kwa wavuaji au wafugaji na kuuza kwa reja reja.
-
Kuuza vifaa vya uvuaji wa samaki kama nyavu, ndoano na vingine.
Kwa kila wazo kuna mengi unaweza kufanya ndani yake na ukaingiza kipato kizuri. Lakini pia yapo mengi ya kujifunza zaidi.
Unapochagua wazo utakalofanyia kazi, wekeza kujifunza kwa kina pia.
Kocha.