Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kipande cha ardhi.
Kama una kipande cha ziada cha ardhi kwenye eneo lako la makazi, unaweza kukitumia kama sehemu ya kuingiza kipato zaidi.
Kulingana na ukubwa wa kipande hicho cha ardhi eneo ulipo, kuna mawazo mbalimbali unayoweza kufanyia kazi.
Hapa kuna mawazo kumi unayoweza kuanza nayo.
- Kujenga nyumba au vyumba kwa ajili ya kupangisha watu kwa makazi.
-
Kujenga vyumba vya biashara na kuvitumia mwenyewe au kuwapangishia wengine.
-
Kufanya kilimo cha kisasa kama kutumia shamba kitalu (greenhouse).
-
Kufanya ufugaji wa kisasa kama wa kuku kwa kutumia vizimba (cages).
-
Kuwa na bustani ya maua ambayo utauza kwa wengine.
-
Kujenga ukumbi wa michezo na/au shughuli mbalimbali.
-
Kuingia makubaliano na wengine wajenga vyumba vya biashara kisha kukatana kwenye kodi, hasa kama huna mtaji wa kufanya hivyo mwenyewe.
-
Kujenga mabwawa ya kufuga samaki.
-
Kujenga mabwawa ya kuzalisha chakula cha mifugo kama azola.
-
Kutengeneza ubunifu wa kuwa sehemu tulivu kwa mapumziko ya watu.
Mawazo haya unaweza kufanyia kazi na kipande cha ardhi unachokiona ni kidogo kikawa na tija kubwa.
Unapochagua wazo la kuanza nalo, jifunze kwa kina, fanya tafiti na ona wapi unakoweza kuanzia.
Kocha.