Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mawazo yako.
Akili unayo na unaweza kuitumia kuzalisha mawazo mbalimbali.
Zipo njia mbalimbali za kuingiza fedha kupitia mawazo yako.
Hapa kuna mawazo kumi ya kufanya hivyo.
- Kuja na mawazo ya kuongeza kipato chako na kuyafanyia kazi.
-
Kuja na mawazo ya kupunguza gharama zako ili kuokoa fedha zaidi.
-
Kutoa mawazo yako kwa wengine na kulipwa pale wanapoyafanyia kazi.
-
Kuandika mawazo yako kwenye kitabu na kuuza kwa wengine.
-
Kuyakatia hatimiliki mawazo yako na kutoa leseni kwa wengine kuyatumia na kukulipa.
-
Kuwasaidia wengine kuweza kuja na mawazo bora na wakakulipa.
-
Kuwa na utaratibu wa kuja na mawazo endelevu ya kuendelea kuboresha kile ambacho unafanya.
-
Kuwa mshauri elekezo kwenye eneo ulilochagua na kila mara kuja na mawazo mapya ya kuwasaidia wale unaowashauri.
-
Kuboresha mawazo ambayo tayari yapo ili yalete tija zaidi.
-
Kuja na mawazo ya kukutanisha pande mbili zinazohitajiana sana ila hazijuani.
Mawazo ni rahisi kupatikana na hivyo hayana thamani sana. Ila unapofanya mawazo kuwa kazo yako kuu, unajisukuma kuja na mawazo bora na ya tofauti, kitu kinachowafanya wengine kuwa tayari kukulipa kwa mawazo yako.
Kocha.