Unapoamua kufanya makubwa na ya tofauti, utajiona kama uko peke yako.

Dunia itaonekana kutokujali kabisa na kusubiri uanguke ili ikucheke. Lakini manbo hayako hivyo, kuna wengi sana ambao wako nyuma yako, japo wapo kimya kimya.

Watu hao wananufaika na kile unachofanya na pia wanapata matumaini ya wao pia kufanya makubwa.

Unapokata tamaa kwenye kile unachofanya haikuathiri tu wewe mwenyewe, inawaathiri wengine wengi pia.

Kila unapojiona mpweke kwenye safari yako ya mafanikio, jikumbushe kuna wengi wako nyuma yako japo huwaoni, hilo litakupa nguvu kubwa ya kuendelea na safari yako.

Ukurasa wa kusoma ni kuna wengi wananufaika japo hawasemi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/16/2420

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma