#SheriaYaLeo (2/366); Rudi Kwenye Ulichopenda Utotoni.

Ulipokuwa mtoto, kuna vitu ulipenda sana kufanya au kufuatilia.
Hata pale ulipokatazwa au kukatishwa tamaa, bado uliendelea kung’ang’ana na vitu hivyo na hukumsikiliza yeyote.

Hilo halikutokea kwa bahati mbaya, bali ilitokana na msukumo wa nguvu kubwa iliyo ndani yako, ambayo ulikuwa unaisikiliza ulipokuwa mtoto.

Lakini kadiri ulivyokuwa unakua, ukaanza kuipuuza nguvu hiyo na kutekwa na mambo mbalimbali ya maisha. Matokeo yake ni umekuwa unahangaika na mengi lakini bado hupati utulivu.

Huu ni wakati wa kurudi kwenye yale uliyopenda utotoni, yale uliyosukumwa zaidi kuyafanya au kuyafuatilia.

Utakaporudi kwenye hayo, nafsi yako inapata ridhiko kubwa na utajua kweli umefika kwenye wito na kusudi lako.

Sheria ya leo; kuna sababu iliyopelekea upende zaidi vitu fulani utotoni. Rudi kwenye vitu hivyo na utagundua wito wako na kusudi la maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma