2503; Kukusanya Na Kutawanya.

Mwanga wa jua ukitawanywa unatoa tu mwangaza wa kawaida.
Lakini mwanga huo huo ukikusanywa eneo moja, unatoa moto mkali wenye kuweza kuunguza chochote.

Nguvu na umakini wako ukivitawanya unaishia kupata matokeo ya kawaida.
Lakini ukikusanya vitu hivyo viwili kwenye maeneo machache, unazalisha matokeo makubwa sana.

Kama huzalishi matokeo makubwa, siyo kwa sababu umekosa nguvu au umakini wa kutosha, bali ni kwa sababu umevitawanya sana vitu hivyo.
Hata pale unapojiambia huna muda, siyo kwamba siku yako ina pungufu ya masaa 24, bali unakuwa umetawanya sana muda wako.

Hatua ya kuchukua;
Kila unapojiambia huna muda au unapoona hujaweza kufanya makubwa, usijiulize umekosa nini, bali angalia umetawanya kiasi gani rasilimali ulizonazo.
Acha kutawanya na anza kukusanya na utabadili matokeo unayoyapata.

Tafakari;
Kwa kutawanya utaweza kugusa mengi, ila kwa madhara kidogo.
Kwa kukusanya utagusa machache, ila kwa madhara makubwa.
Mafanikio hayatokani na mguso, bali madhara.

Kocha.