#SheriaYaLeo (8/366); Kubali Na Ishi Utofauti Wako.

Kila mtu ana utofauti fulani ambao upo ndani yake.
Kuna namna ya ufanyaji wa mambo ambayo ni ya tofauti kabisa.
Na pia kuna vitu vya tofauti kabisa vinavyomvutia mtu tofauti na wengine.

Kwa walio wengi huwa wanapuuza utofauti wao na kuchagua kufanya yale yanayofanywa na wengine.
Kufanya hivyo hupelekea wengi kuwa kawaida na kutokufanikiwa.

Kila aliyefanikiwa kuna kitu cha tofauti kabisa ambacho kimekuwa kinamvutia na amekuwa anakifanya.
Pamoja na kuwa siyo kitu maarufu au kinachoonekana kuwa na manufaa, kadiri mtu anavyokipokea na kuzifanyia kazi, anazalisha thamani ya tofauti kabisa, kitu kinachompa mafanikio makubwa.

Sheria ya leo; Kubali utofauti wako. Tambua kile kinachokutofautisha na wengine na ukiishi hicho. Hivyo ndivyo unavyoweza kuzalisha matokeo ya tofauti na kufanya makubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma