#SheriaYaLeo (12/366); Kikwazo Ndiyo Njia.
Baadhi ya watu huwa inawawia vigumu kujua wito na wajibu wa maisha yao.
Wakati watu wengine wana vitu ambavyo kwao ni rahisi kufanya na hivyo kuwa sehemu ya wito, wao wanakuwa hawana kitu cha aina hiyo.
Kwa hali hiyo wanaweza kufikiri wao hawana wito au wajibu.
Lakini hilo siyo kweli.
Kwani watu hao huwa wana vikwazo fulani kwenye maisha yao ambavyo vinaonekana ni sababu ya kutokupiga hatua.
Lakini wao wanapambana na kuvuka vikwazo hivyo kisha kuweza kufanya makubwa sana.
Kuvuka vikwazo hivyo inakuwa ndiyo wajibu na kusudi la maisha yao.
Kwani wanapovuka vikwazo hivyo, wanatoa njia kwa wengine pia kuweza kuvuka vikwazo vya aina hiyo pia.
Wakati mwingine wanatoa suluhusho ambalo linakuwa na manufaa kwa walio wengi.
Kama umejaribu njia zote za kujua wito na kusudi lako ila hujaweza kujua, angalia ni kikwazo gani kikubwa ulichonacho kwenye maisha yako, kisha kigeuze hicho kuwa ndiyo njia na wajibu wa maisha yako.
Sheria ya leo; Kabiliana na moja ya vikwazo ulivyonavyo kwenye maisha yako. Angalia namna unaweza kukivunja, kukivuka au kukizunguka ili kuweza kupata unachotaka. Usikimbie kikwazo chochote ulichonacho, kimetengenezwa kwa ajili yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma