#SheriaYaLeo (14/366); Epuka Njia Ya Uongo.

Njia ya uongo ni ile ambayo inatuvutia kwa sababu zisizo sahihi – fedha, umaarufu, kuwaridhisha wengine na kadhalika.
Sababu hizo zinakusukuma kufanya kitu ambacho siyo sahihi kwako, ambacho kinakuzuia usiishi kusudi na wajibu wako.

Kama unafanya kwa ajili ya umaarufu, unaishia kuona utupu ulio ndani yako, ambao unajaribu kuujaza na umaarufu huo lakini hilo halitokei.
Kwa sababu unachokuwa umechagua hakiendani na asili yako ya ndani, hupati ridhiko unalotaka kupata.
Kazi yako inaathirika sana na hata umaarufu unaokuwa umeanza kupata, unaanza kupotea, kitu kinachoumiza zaidi.

Kama ni fedha ndiyo zimesukuma maamuzi yako, unajikuta ukifanya kwa hofu na kutaka kuwaridhisha wengine, hasa wazazi.
Hilo hukupeleka kwenye mambo yasiyo sahihi kwako hivyo huridhiki.

Unapojikuta kwenye njia isiyo sahihi una mikakati miwili ya kuondoka;
Moja ni kutambua kwamba umechagua kazi yako kwa sababu zisizo sahihi. Hili unapaswa kufanya mapema kabla hujakutana na anguko.
Mbili ni kukataa na kuasi mapema kabisa dhidi ya nguvu zote zinazokupeleka kwenye njia isiyo sahihi.

Kataa kabisa kufanya kitu kwa sababu ya fedha au umaarufu.
Zikatae nguvu zote zinazokusukuma kwenda kwenye njia isiyo sahihi kwako, hata kama ni wazazi wako.
Unapaswa kuchagua njia sahihi kwako hata kama itahitaji usimame peke yako.

Sheria ya leo: Kama upo kwenye njia ambayo siyo sahihi kwako, ondoka kwenye njia hiyo haraka. Pata nguvu kwenye kukataa na kuasi na itumie kwenda kwenye njia sahihi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma