2513; Ubinafsi wa watu.

Watu watakujali na kuwa wema kwako pale wanapokuwa na kitu wanachokihitaji kutoka kwako.
Pale unapokuwa una matumizi kwao, watakujali sana.

Lakini unapokuwa huna manufaa kwao, wanapokuwa hawana chochote wanachohitaji kutoka kwako, hawatakujali wala kuwa wema kwako. Watakudharau na kukupotezea.

Hilo linaweza kukuumiza, kukukasirisha na kukufanya uwe na chuki.
Lakini hayo yote hayatabadili tabia za asili ambazo watu wanazo.
Watu wana mambo mengi kiasi kwamba wanahitaji kuweka vipaumbele vyao kulingana na mahitaji yao.

Hatua ya kuchukua;
Mara zote kuwa mwema na wa kujali kwa wengine. Fanya kile chenye manufaa kwa wengine.
Watu wanapokujali na kuwa mwema kwao furahia hilo, maana kuna namna wananufaika.
Na pale wanapokupotezea na kutokukujali usiumizwe sana na hilo, jua kuna wakati watakuja watakapokuwa na uhitaji.
Wewe wajibu wako ni kutoa thamani kubwa kwa wengine, bila ya kujali wanaipokeaje.

Tafakari;
Swali la kwanza ambalo watu hujiuliza kabla ya kufanya chochote ni MIMI NANUFAIKAJE KATIKA KUFANYA HILI. Ukiweza kuwaonyesha watu manufaa watakayopata kwa kushirikiana na wewe, utawapata kwa wingi.

Kocha.