#SheriaYaLeo (17/366); Chanzo sahihi cha ubunifu.
Unapaswa kubadili dhana yako ya ubunifu na kuuangalia kwenye kona mpya.
Mara nyingi watu huhusianisha ubunifu na akili au namna fulani ya kufikiri.
Ukweli ni kwamba ubunifu ni kitendo kinachohusisha nafsi yako nzima – kuanzia hisia, nguvu, tabia na fikra.
Kuja na uvumbuzi mpya, kutengeneza kitu kinachowagusa watu na kuzalisha matokeo yoyote ya tofauti kunahitaji muda na juhudi.
Hilo linahitaji miaka mingi ya kufanya majaribio na kukutana na vikwazo mbalimbali. Utaanguka na kushindwa lakini utapaswa kuweka umakini wako kwenye kile unachofanya.
Unapaswa kuwa na subira pamoja na imani kwamba kile unachofanya kitazalisha matokeo mazuri.
Unaweza kuwa na fikra zenye akili sana, zenye ujuzi na mawazo bora na ya kipekee. Lakini kama utachagua kufanyia kazi kitu kisicho sahihi kwako, utaishia kupoteza nguvu hizo na hutazalisha matokeo yoyote makubwa.
Utapoteza bure nguvu na akili zako.
Sheria ya leo; Fanyia kazi kile kinachounganisha nafsi yako yote, kikigusa kila eneo lako na mawazo bora yatakuja kwako na kuweza kufanya makubwa na ya kibunifu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma