2516; Makosa yanayojirudia rudia.
Kwenye kazi au biashara unayoifanya, kuna makosa huwa yanajirudia rudia kila mara.
Unaweza kulalamikia makosa ya aina hii, lakini ni fursa nyingine nzuri ya kuboresha kile unachofanya na kujenga mfumo unaozuia hayo yasijirudie.
Kwa kila kosa linalojirudia rudia, kaa chini uandike nini kinafanya kosa hilo lijirudie na namna gani unaweza kufanya ili lisijirudie tena.
Hicho unachoandika unakuwa ndiyo mfumo unaotumika ili kuzuia kosa husika lisiendelee kuwa kikwazo.
Ukichagua kufanya hivi kwa kila kosa linalojirudia, utaweza kutatua mengi na hata kutengeneza mfumo mzuri wa kufanya kile unachofanya.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kila kosa linalojirudia kutokea, kaa chini na uandike namna ya kulizuia lisitokee au kulikabili baada ya kutokea. Kisha elekeza watu wote wanaohusika namna ya kuchukua hatua hizo. Na hapo unakuwa umeanza kujenga mfumo wa kile unachofanya.
Tafakari;
Kosa linalojirudia rudia siyo changamoto bali ni uzembe. Usikubali uzembe uwe kikwazo kwako, chukua hatua sahihi.
Kocha.