#SheriaYaLeo (20/366); Ona Ubobezi Kama Ukombozi.
Dunia imejaa matatizo mbalimbali, na sehemu kubwa ya matatizo hayo tumeyatengeneza wenyewe.
Kutatua matatizo hayo kunahitaji juhudi na ubunifu mkubwa.
Kutegemea mazoea, teknolojia na kuwa mwema haitatusaidia.
Tunahitaji nguvu ya kuweza kuyatambua matatizo hayo na kutengeneza taasisi mpya zinazoweza kukabiliana na mabadiliko tunayopitia.
Ni lazima tutengeneze ulimwengu wetu wenyewe la sivyo tutakufa kwa kushindwa kuchukua hatua.
Tunahitaji kurudi kwenye dhana yetu ya ubobezi, ambayo inatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine.
Huu siyo ubobezi kwa ajili ya kuitawala asili au kuwatawala wengine, bali kuamua hatima yetu.
Kuishi tu kwa mazoea hakuna manufaa yoyote, bali ni kujijaribia maisha mwenyewe.
Unapaswa kuwa mfano wa nini kinaweza kufikiwa kupitia ubobezi. Unachangia kwenye hitaji muhimu la maendeleo makubwa ya jamii ya binadamu.
Lazima uelewe kwamba watu hupata ubora wa akili wanayostahili kupitia hatua wanazochukua.
Sheria ya leo; Unapaswa kuona mpango wako wa kufikia ubobezi kama kitu muhimu kabisa na chanya kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma