#SheriaYaLeo; Badilika kuanzia ndani kidogo kidogo.

Sisi binadamu huwa tunahangaika na yale tunayoweza kuona kwa macho yetu.
Tunapoangalia mabadiliko kwenye maisha ya wengine, tunaona bahati nzuri ambayo mtu aliipata kwa kukutana na mtu aliyemsaidia sana.
Tunaona miradi iliyomletea mtu fedha na umaarufu.
Kwa maneno mengine tunaona manadiliko yanayoonekana kwa nje.

Kwa uhalisia, kinacholeta mabadiliko hayo makubwa ya nje ni mabadiliko madogo madogo yanayokuwa yametokea ndani ya mtu.
Hatua ambazo mtu amechukua kujijengea ujuzi na uzoefu, kuboresha nidhamu yake ya kazi na kuweza kuhimili ukosoaji ni mabadiliko ya ndani ambayo siyo rahisi kuyaona.
Mabadiliko yoyote yanayoonekana kwa nje ni udhihirisho wa maandalizi yaliyokuwa yanaendelea ndani yake kwa muda mrefu.

Kwa kupuuza mabadiliko hayo makubwa ya ndani, tunashindwa kuleta mabadiliko yoyote makubwa ndani yetu. Na hilo linapelekea kufikia ukomo wa mafanikio ndani ya muda mfupi.
Hilo linatupa msongo, tunahangaika kutafuta mabadiliko ya nje ambayo ni ya muda mfupi na hayadumu.
Hilo linakuwa likijirudia mara kwa mara kwenye maisha yetu.

Njia ya kuleta mabadiliko ya uhakika na yenye tija ni kuacha kuangalia yale ambayo watu wanasema au wanafanya. Kuacha kuangalia fedha, umaarufu au mwonekano wa nje wa vitu. Badala yake angalia ndani, angalia mabadiliko madogo ya ndani ambayo yamejenga msingi wa mabadiliko makubwa yanayoonekana nje.
Kwa kujua nguvu ya mabadiliko madogo madogo ya ndani na kuifanyia kazi, utaweza kutengeneza mabadiliko makubwa kwa nje, yenye tiba na yanayodumu muda mrefu.

Sheria ya leo; Ni kitu gani upo tayari kukifanyia kazi hata kama hakuna mtu anayeona? Kama fedha isingekuwa tatizo, kipi ungehangaika nacho? Ni yale unayoyajali kweli kutoka ndani yako ndiyo yenye nafasi ya kukuwezesha kufanya makubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#Ubunifu