#SheriaYaLeo (28/366); Njia haijanyooka.
Wakati unaianza safari yako ya wito na kusudi la maisha yako, unachagua eneo linaloendana na yale yaliyo ndani yako.
Sehemu unayoanzia inakupa nafasi ya kujifunza na kujijengea ujuzi na uzoefu muhimu.
Pia inakupa nafasi ya kuingiza kipato na kujijengea kujiamini.
Kadiri unavyokwenda unagundua kuna njia za pembeni ambazo zinakuvutia zaidi, wakati njia nyingine zikiwa hazikuvutii.
Unaendelea kubadilika kadiri unavyokwenda, kwa kutanua ujuzi na uzoefu wako.
Mwishowe unafika eneo au kukutana na fursa ambayo inakufaa vizuri zaidi. Utaitambua kwa namna itakavyoibua shauku kubwa ndani yako na kujua ndiyo kitu sahihi kwako.
Baada ya kufika eneo hilo, kila kitu kitakaa sehemu yake.
Utajifunza kwa haraka na kwa kina.
Ujuzi wako utafika ngazi ambayo unakuwa huru kuondoka kwenye kundi lolote ulilopo na kufanya mambo yako peke yako.
Kwenye dunia ambayo mambo mengi yako nje ya udhibiti wako, hilo litakupa wewe nguvu na mamlaka makubwa.
Utaamua mambo yako mwenyewe na hutakuwa tena chini ya wengine ambao wanakuwa na ajenda zao binafsi.
Sheria ya leo; Unapaswa kuiona kazi au biashara yako kama njia yenye kona nyingi na siyo iliyonyooka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#Ubunifu