#SheriaYaLeo (30/366); Amini kwenye mchakato.

Unapoanza kufanya kitu chochote kile kipya kwako, unakutana na ugumu mkubwa.
Unakua hujui mambo mengi kuhusu kitu hicho na hivyo unasumbuka sana mwanzoni.

Unaweza kukata tamaa kwa kuona vitu ni vingi na vigumu, huwezi kupambana navyo.
Kama utakata tamaa, utakuwa umeishia hapo na kushindwa kufikia ubobezi.

Lakini kama utaacha kuangalia ugumu ulio mbele yako na kufanyia kazi mchakato wa kujifunza na kuchukua hatua, utazidi kujijenga kadiri unavyokwenda. Utapata uelewa mkubwa pamoja na kujiamini kadiri unavyoelewa kile unachofanya.

Utakavyozidi kukaa kwenye mchakato utafikia ubobezi wa juu kabisa na kuweza kufanya kwa viwango vya tofauti na wengine wanavyofanya.

Sheria ya leo; Mwanzo huwa ni mgumu, unapoamini kwenye mchakato na kujipa muda, utaweza kuvuka ugumu huo na kufikia ubobezi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu