Karibu mwanamafanikio kwenye kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA.
Kwenye kipindi hiki unakwenda kujifunza mengi kwa kina kama ifuatavyo.
Kwenye somo la juma tunajifunza jinsi ya kupata hamasa isiyoisha ili uweze kuyafanyia kazi malengo yako bila kurudi nyuma. Hapa utajifunza hatua tano za kuchukua kwenye kila siku yako ili kuchochea hamasa yako.
Kwenye kitabu cha juma utajifunza dhana kuu ya udhibiti na usimamizi mzuri wa muda wako ambayo ni muda tayari una ukomo huku mambo ya kufanya yakiwa mengi. Kwa kukubali ukomo huo wa muda na kuchagua yapi unafanya na yapi hufanyi itakusaidia sana kuweza kutumia muda vizuri na kufanya yenye tija.
Kwenye mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Regina Panga anatushirikisha yale aliyojifunza kwenye maisha yake na safari ya mafanikio. Anatushirikisha fursa kwenye kilimo cha miti, jinsi anavyokabiliana na changamoto ya kuwa na mtoto mwenye ulemavu na jinsi alivyovuka hofu ya kuanza biashara.
Kupitia mjadala wa wote kuna ushauri mzuri sana ambao umetolewa na wanamafanikio walioshiriki mjadala.
Hiki ni kipindi muhimu sana kusikiliza maana kina mengi ya kujifunza kwenye kila eneo la maisha.
Tenga muda sasa na usikilize kipindi hiki, ujifunze na kwenda kuchukua hatua ili maisha yako yaweze kuwa bora zaidi.
Kila la kheri.
Kocha.