#SheriaYaLeo (38/366); Njia pekee ya mkato ya kufika kwenye ubobezi.
Maisha ni mafupi na muda wako wa kujifunza na ubunifu una ukomo.
Bila ya kuwa na mwongozo, utapoteza miaka yako ya thamani ukijariby kujifunza kutoka vyanzo mbalimbali na bado usifikie ubobezi.
Badala ya kufanya hivyo, unapaswa kufuata mfano wa wabobezi waliopita, ambao walitafuta mamenta wazuri na kujifunza chini yao.
Kuwa na menta ndiyo njia bora kabisa ya kujifunza na kujijengea ubobezi.
Menta sahihi anakuwa anajua wapi mtu anapaswa kuweka nguvu na umakini wake ili kujijengea ujuzi na kuweza kufanya makubwa.
Menta anakupa changamoto za kukusukuma kukua zaidi na anakupa mrejesho wa moja kwa moja kwenye kila hatua unayopiga.
Kwa kuwa unafanya kazi kwa karibu kabisa na menta, anakuwa anakujua vizuri na wewe kumjua vizuri.
Kwa yeye kukujua anakuongoza kuwa bora zaidi.
Na kwa wewe kumjua unajifunza mengi kutoka kwake, kuanzia namna ya kufikiri na kuchukua hatua sahihi.
Unapaswa kuchagua menta sahihi kwako, anayeendana na kile unachotaka kubobea.
Ukishamchagua menta jifunze chini yake mpaka ufikie ubobezi kama wake.
Kisha baada ya hapo ondoka chini yake ili uweze kufikia ubobezi wa juu zaidi.
Lengo lako ni kuhakikisha unafikia ubobezi wa juu kuliko hata menta wako.
Sheria ya leo; Kuchagua menta sahihi ni sawa na kuweza kuwachagua wazazi wako; uchaguzi mbaya ni hatari kubwa kwako.
#NidhamuUadilifuKujifuma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu