#SheriaYaLeo (39/366); Menta Sahihi Kwako.
Kupata menta sahihi kwako, angalia mtu ambaye kazi zake zinakuvutia sana, zinakupa hamasa na msukumo wa kuwa kama wao.
Angalia mtu ambaye mtindo wake wa maisha na kazi anazofanya unakupa shauku kubwa, unajiona unaweza kufanya kwa namna kama yake.
Pia angalia ni mtu wa aina gani unataka kuwa miaka 10 inayo, kisha tafuta mtu ambaye ameshakuwa hivyo na ujifunze kupitia yeye.
Kupata menta sahihi ni hatua ya kwanza na muhimu ha kufika kwenye ubobezi.
Hivyo hakikisha unampata menta sahihi kwako.
Sheria ya leo; Pata menta sahihi kwa kuangalia mtu ambaye kazi yake inakuhamasisha, mtindo wake unakupa shauku na unajiona ukiwa kama yeye miaka 10 inayo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu