#SheriaYaLeo (40/366); Raha itokane na unachofanya.
Kadiri unavyoendelea kujifunza na kujijengea ujuzi wako, unaendelea kubadilika na kuwa bora zaidi.
Unagundua uwezo mkubwa ulio ndani yako ambao ulikuwa umelala, ambao unaamshwa kadiri unavyokwenda.
Unakua kiakili na kihisia na maana ya raha kwako inabadilika.
Vitu vinavyotoa raha ya haraka kama ulevi mitandao na mengine yanaonekana kuwa usumbufu kwako ambao unakupotezea muda bila ya kuwa na manufaa yoyote.
Raha ya kweli kwako inatokana na kile unachofanya, pale unapovuka magumu na changamoto mbalimbali, unapojijengea ujuzi, kujiamini na uzoefu mkubwa kwenye kile unachofanya.
Unajijengea uvumilivu mkubwa na uchoshi hauwi msukumo kwako kutafuta usumbufu, bali hitaji la changamoto mpya ya kuitatua.
Sheria ya leo; Raha kwako inapaswa kutokana na kile unachokifanya, ili ukipe kipaumbele kikubwa kuliko vingine vyote. Hapo hutasumbuliwa na raha za nje ambazo hazina mchango wowote kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu