#SheriaYaLeo (48/366); Ukweli Unaouma.
Hakuna njia ya mkato ya kufika kwenye ubobezi.
Hakuna namna unaweza kukwepa mafunzo na ufanyaji wa kina wa kile unachotaka kubobea.
Hayo yanahitaji muda ambao hauwezi kuharakishwa kwa namna yoyote ile.
Kwa wastani, inachukua angalau miaka 10 ya kujifunza na kufanya kwa kina ndiyo mtu aweze kufikia ubobezi.
Kwa asili, ubongo wetu binadamu huwa unahitaji kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu ili kuweza kukielewa kwa kina na kuweza kufikia ubobezi wa hali ya juu.
Hakuna namna ya kufupisha mchakato huo na bado ukaweza kufikia ubobezi.
Ni kawaida kwetu binadamu kutafuta njia za mkato za kupata kile tunachotaka.
Kitendo tu cha kutafuta njia ya mkato kwenye ubobezi ni kiashiria kwamba mtu hawezi kufikia ubobezi anaoutafuta.
Sheria Ya Leo; Hakuna namna unaweza kukwepa mchakato mrefu wa mafunzo ya kufikia ubobezi. Achana kabisa na tamaa ya kutafuta njia za mkato.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu