2550; Mtu rahisi kumdanganya.
Mtu rahisi kabisa kumdanganya kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe.
Unaya ni hutajua wakati unajidanganya, ni mpaka baadaye sana na mambo yakiwa yameshaharibika ndiyo unagundua ulikuwa unajidanganya.
Kwanza, kama unataka sana kitu kiwe kweli au kiwe sahihi kwako, hayo ndiyo utakayoona.
Kutakuwa na viashiria kama kitu siyo kweli au siyo sahihi, lakini kwa sababu unataka sana kiwe kweli na sahihi, hutaviona.
Utaona kile unachotaka sana kuona na ni mpaka ukweli uje ukukamate ndiyo utazinduka kutoka kwenye usingizi wa kujidanganya.
Pili, pale unapoamini huwezi kukosea au kukosa kile unachotaka, akili hayo haitakuruhusu uyaone makosa. Kadhalika utatumia kila njia hata kama siyo sahihi kupata unachotaka. Yote hayo yanazidi kuharibu na kuwa kikwazo kwenye kile unachotaka.
Kuondokana na hali hii ya kujidanganya, kwa kila unachokubaliana nacho tafuta hoja za kukipinga. Tafuta hoja nzito kwa nini unachoamini ni kweli siyo kweli, au ni sahihi siyo sahihi.
Kama huwezi kupata hoja yoyote kwa nini unachokubaliana nacho siyo sahihi, basi jua kuna mahali unajidanganya.
Kama kila kitu unaona kipo sawa kabisa, umenasa kwenye mtego wa kujidanganya wewe mwenyewe.
Na ni bora usiendelee kwanza mpaka upitie kila kitu kwa kina.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kila maamuzi unayoyafanya kwenye maisha yako, jiulize ni kwa namna gani umejidanganya katika kufikia maamuzi hayo. Siyo kama umejidanganya, ni umejidanganya.
Kisha pitia kila hatua ya maamuzi na kuona namna ambavyo umejidanganya.
Ni vigumu sana kufikia maamuzi yoyote yale bila kujidanganya, ubaya siyo kujidanganya, bali kujidanganya bila kujua.
Tafakari;
Kuna kiwango cha kujidanganya na kupuuzia unachokihitaji kwenye maisha yako ili yaweze kwenda. Muhimu ni ujue kabisa wapi unajidanganya na wapi unapuuzia. La sivyo utajipa kichwa na kwenda kukutana na anguko kubwa.
Kocha.
Asante Sana kocha wangu.
LikeLike
Karibu.
LikeLike