#SheriaYaLeo (54/366); Usitosheke na maarifa.
Ili kufikia ubobezi wa hali ya juu na kudumu kwenye ubobezi huo, hupaswi kuridhika na maarifa.
Hupaswi kufika mahali na kuona tayari umeshajifunza vya kutosha na kujua kila kitu.
Kila wakati unapaswa kuwa na njaa na kiu ya kuendelea kujifunza kwa kina zaidi.
Jifunze kwa undani na kwa kasi kubwa kuliko wengine.
Kuwa na udadisi mkubwa na nenda zaidi ya unavyofundishwa au unavyotegemewa kujifunza.
Maarifa yote unayoendelea kuyapata hayawi tu ya bure.
Bali yanakupa manufaa ya ziada, ambayo wengine hawana.
Yanakuwezesha kuziona na kuzitumia fursa ambazo watu wengine hawazioni au hawawezi kuzitumia.
Siku utakayojiambia umeshajua kila kitu au huna tena kipya cha kujifunza, ndiyo siku utakayokuwa umekaribisha anguko kubwa.
Sheria ya leo; Pata raha ya kipekee kwenye kujifunza kwa kina. Kamwe usiridhike na kutosheka na maarifa uliyonayo, endelea kupata mengi zaidi na zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu