#SheriaYaLeo (55/366); Mpite Mwalimu Wako.
Unapoanza kujifunza kwenye eneo unalotaka kubobea, unapaswa kufuata maelekezo unayopewa na mwalimu wako, ambaye tayari ameshabobea kwenye eneo hilo.
Ukishaijua misingi yote muhimu ya eneo hilo ulilochagua, unapaswa kujifunza zaidi ya kile ambacho mwalimu wako anakufundisha.
Unapaswa kuyageuza mafunzo yake yaendane na upekee na utofauti wako.
Unapaswa kujaribu vitu vipya na vya kipekee kabisa kwako.
Lengo ni uweze kufikia ubobezi wa hali ya juu kabisa, uweze kumpita hata mwalimu wako.
Kuendelea kubaki chini ya mwalimu wako kwa miaka yote ni kutokutendea haki mafunzo unayoyapata na uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Mwalimu anakuonyesha na kukuongoza njia pale unapoianza safari.
Ni wajibu wako kutengeneza njia ya kipekee kwako kadiri unavyoendelea kubobea.
Sheria ya leo; Tambua kivuli cha ubobezi wa menta au mwalimu uliyechagua kujifunza kwake. Hakikisha hubaki chini yake kwa maisha yako yote, badala yake unajitofautisha na kujijengea ubobezi wa kipekee kwako. Lengo ni kuwapita wengine wote kwa kuwa wewe halisi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu