#SheriaYaLeo (59/366); Kata yasiyokuwa na umuhimu.

Kwenye safari yako ya ubobezi, utakutana na mengi kutoka kwa wale ambao unajifunza kwao.
Watakuwa na mengi ya kukufundisha na kukutana uyachukue yote kwa sababu ni muhimu.

Lakini siyo yote yanayoweza kuwa na umuhimu kwako.
Hivyo wewe unapaswa kuchagus yale muhimu yanayokufikisha wewe kwenye ubobezi wa hali ya juu kabisa na kuyapa mkazo zaidi.
Mengine yote yakate, achana nayo ili yasiwe kikwazo kwako kufikia ubobezi.
Maana kuhangaika na mambo mengi kwa wakati mmoja ni kujizuia kufikia ubobezi.

Kuna hatua utafikia ambapo utahitaji pia kumkata yule unayejifunza kwake.
Pale unapokuwa umefikia ubobezi kiasi kwamba huna tena cha kujifunza kutoka kwake.
Pale unapotaka kujaribu vitu vipya na vya kipekee kabisa kwako.

Safari ya kuelekea kwenye ubobezi inahitaji uasi.
Na siyo uasi mbaya, bali uasi mzuri, wa kuondoka chini ya wengine na kujisimamia wewe mwenyewe.
Uasi ndiyo unaokutambulisha wewe kwa wengine, kupitia kuanzisha mtindo na namna yako ya kipekee ya kufanya mambo.

Sheria ya leo; Chukua yale ambayo ni muhimu na yanayokufaa kutoka kwa wale unaojifunza kwao. Kata mengine yote ambayo hayana umuhimu.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu