#SheriaYaLeo (61/366); Endelea kutanua akili yako.

Kadiri unavyobobea ndivyo unavyoshawishika kwamba umeshajua kila kitu na hakuna kipya cha kujifunza.

Lakini ubobezi huwa hauendi hivyo, ubobezi hauna kilele.
Ubobezi ni zoezi endelevu.
Siku utakayoona umeshafika kwenye kilele ndiyo siku ambayo utaanza kuanguka.

Hivyo kwenye safari yako ya ubobezi, bila ya kujali umefika wapi, endelea kutafuta ubobezi zaidi.
Endelea kujifunza na kutanua akili yako.
Endelea kujaribu vitu vipya kadiri unavyokwenda.

Maisha ni mwendo, kama huendi mbele basi unarudi nyuma, hakuna kusimama.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye ubobezi, kama huendelei kubobea zaidi basi unapoteza ubobezi ulionao.

Mara zote jifunze na kujaribu vitu vipya, ili kubobea zaidi kwenye kile unachofanya.
Jifunze mambo yanayoendana na kile ulichobobea, ili kutanua wigo wako na kupata fursa nyingi zaidi.

Sheria ya leo; Endelea kutanua akili yako kwa kupata maarifa na ujuzi zaidi kwenye kile unachobobea na mengine yanayohusiana na kitu hicho. Kamwe usiridhike na kuona umeshafika kileleni, safari ya ubobezi haina kilele.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu