2577; Msukumo wa ndani.
Kama mtu anataka kweli kufanya kitu, hakuna chochote cha nje kinachoweza kumzuia.
Na kama mtu hataki kabisa kufanya kitu, hakuna chochote cha nje kinachoweza kumlazimisha.
Kila kitu kinaanzia kwenye msukumo wa ndani ambao mtu anao.
Bila ya msukumo huo wa ndani, hakuna hatua zozote ambazo mtu anaweza kupiga.
Unapotafuta watu wa kujihusisha au kushirikiana nao kwa namna yoyote ile, angalia kwanza msukumo ulio ndani yao.
Kama inabidi uwasukume na kuwalazimisha kila wakati, jua siyo watu sahihi kwa kitu hicho.
Kadhalika kwako mwenyewe, hakikisha chochote unachofanya kuna msukumo mkubwa kutoka ndani yako.
Kama inabidi usukumwe na kulazimishwa na wengine, kama unatumia nguvu kubwa sana, jua hicho siyo kitu sahihi.
Kikwazo kikubwa cha mafanilio kwa walio wengi ni kukosa msukumo wa ndani kwenye kile walichochagua kufanya.
Wewe epuka kikwazo hicho kwa kuchagua kitu ambacho ndani yako kuna msukumo mkubwa wa kukifanya.
Hatua ya kuchukua;
Ndani yako kuna msukumo mkubwa kwenye baadhi ya vitu na maeneo fulani. Msukumo huo huwa haupotei hata kama usipoutumia.
Ni wajibu wako kujua msukumo wako upo kwenye vitu na maeneo gani kisha kuutumia.
Tafakari;
Kila mmoja ana moto ndani yake, ni moto huo ndiyo unaoweza kumfikisha kwenye mafanikio makubwa.
Zindua moto wako ili ukuwezeshe kufanya makubwa.
Kocha.